Search This Blog

Sunday, June 20, 2010

Umuhimu wa Uzazi wa Moango

Source:RK,LM (mpango wa Uzazi)
ED:
DATE: 09/06/2010
KAHAMA.
Baadhi ya wanawake walioanza kutambua umhimu wa uzazi wa mpango wilayani Kahama mkoani Shinyanga wamebainisha kuwa suala la uzazi usio wa mpango ni moja ya kikwazo kikubwa cha wao kutopata fursa ya kujihusisha na masuala ya kiuchumi

Bi.Ester Ngasa ni mkazi wa mjini Kahama na ambaye ni mmoja kati ya watu ambao kwa sasa anatambua umhimu wa kujiunga na uzazi wa mpango na kuwa miongoni wa watu wanaoweza kuhubiri faida za uzazi wa mpango katika suala zima la uzalishaji mali

Akizungumza na mwandishi wa makala haya Bi.Ester anaeleza kuwa baada ya kuelimishwa na kutambua umhimu wa uzazi wa mpango elimu aliyopata katika hospitali ya wilaya kupitia mpango wa uzazi chini ya Engenderheath kwa ufadhili wa watu wa marekani ameamua kumshirikisha mumewe ili wajiunge katika mpango huo

CUE IN---“ndiyo tulielewana na ndio maana mimi nikaanza…………

Bi Betha Julius ni mmoja wa watu waliokubali mpango huu wa uzazi wa mpango unaofadhiliwa na serikali ya watu wa Marekani na kuanza kuutumia ambapo akizungumzia zaidi mpango huu anabainisha jinsi ambavyo mtu anaweza akunufaika na mpango wa uzazi wa mpango

CUE IN: unazaa kwa wakati unaotaka mwenyewe…..

Naye Bi.Devotha Rutaiwa ni muuguzi katika hospitali ya wilaya ya Kahama ambaye pia ni mmoja kati ya watu waliopo katika mpango wa kuhamasisha uzazi wa mpango anaeleza jinsi hali ilivyokuwa wakati walipokuwa wakiaanza hamasa ya uzazi wa mpango wilayani Kahama
CUE IN: zamani tulikuwa tunapata wateja wachache ……..

Dr.Helen Yesaya ni mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya Kahama ambaye hapa anaeleza njia mbalimbali zinazotumika katika suala zima la uzazi wa mpango na njia zipi ambazo waliowengi wamekuwa wakizipendelea
Cue in: sisi tuna njia nyingi za uzazi wa mpango hapa kuna sindano………

Mwalimu Kalile toka shule ya msingi Busungu ni mmoja kati ya wanaume wachache ambao wameukubali mpango wa uzazi wa mpango na akiwa katika foleni ya kusubiri kufunga uzazi na maelekezo mbalimbali yahusuyo uzazi wa mpango anaeleza jinsi anavyoziona faida za uzazi wa mpango na kubainisha baadhi ya madhara ya uzazi usiozingatia masharti ya uzazi wa mpango

Cue in: katika ngazi ya familia uzazi wa mpango ni mhimu sana kwa maana kwamba kulingana na hali ya sasa hivi kiuchumi inawapain sana……

Hata hivyo wanawake waliowengi katika mazungumzo yao na mwaandishi wa makala haya walionesha kuwa wanahamu kubwa ya kutaka kujihusisha na masuala mengine ya uzalishaji mali katika jamii lakini kikwazo kikubwa ni mzigo mkubwa wa familia ambapo wanaume hubakia na jukumu la uzalishaji mali hali inayodaiwa wakati fulani kuleta manyanyaso kwa wanawake

Aidha mpango huu wa Engenderheath unaofadhiliwa na watu wa marekani kwa ushirikiano na serikali unatajwa kuwa na umhimu mkubwa sana kuleta hali ya wanafamilia kujitambua katika suala zima la uzazi ili kuweza kunufaika na faida za uzazi wa mpango hususa ni katika nyaja za kiuchumi

Katika suala zima la kuwa na afya njema kwa akina mama ni suala ambalo linaelezwa kuwa kupitia uzazi wa mpango wanaweza kuwa na afya njema zaidi kwani kunakuwa na matibabu na ushauri wa mara kwa mara kuhusiana na afya ya uzazi

EndS

No comments: