Search This Blog

Msongamano umepungua

akina baba waliowasindikiza wake zao clinic wanawasubiri nje ya zahanati ili warudi nao nyumbani. Isagehe Zahanati, Kagongwa wilayani Kahama

akina mama wakisubiri huduma ya uzazi wa Mpango katika zahanti ya Isagehe, Igongwa Kahama

Emmanuel Chacha

Kahama

Tatizo la msongamano wa wagonjwa katika Wodi ya Wanawake katika Hospitali ya wilaya ya Kahama imepungua baada ya kuanzishwa kwa kitengo maalumu cha kuhudumia wanawake wanaoharibikiwa mimba.
Muuguzi Mfawidhi wa wodi hiyo Bibi Valelia Mwaja amesema kuwa kabla ya kuanzishwa kwa huduma hiyo mwaka 2008 wanawake walioharibikiwa mimba walikuwa wakisubiri kuhudumiwa katika wodi ya upasuaji.
Aidha amesema kuwa kuanzishwa kwa huduma hiyo katika baadhi ya zahanati na vituo vya afya hasa katika maeneo ya vijijini kumepunguza idadi ya wanawake walioharibikiwa mimba ambao wanakwenda katika hospitali hiyo ya wilaya.
Ameoongeza kuwa mbali na kuwasafisha wanawake walioharibikiwa mimba, kitengo hicho pia huwapa elimu afya ya uzazi, uzazi wa mpango na magonjwa ya zinaa ikiwemo maambukizi ya virusi vya ukimwi.