Na Emanuel Jacob Ndosi.Radio Fadeco Karagwe
Imeelezwa kuwa endapo mila na desturi za zamani zitatumika kikamilifu katika kuhimiza maadili kwa vijana tatizo la mimba za utotoni wilayani Karagwe mkoni Kagera litamalizika au kupungua.
Hayo yameelezwa na baadhi ya wananchi wa wilaya hiyo katika utafiti uliofanywa na kundi la waandishi wa habari chini ya ufadhili wa shirika la Utu mwanamke ili kubaini njia bora zinazoweza kutatua tatizo hilo kwa wasichana.
Bi.Frolence Anatory Mkazi wa kijiji cha Nyaboigwera kata ya Ndama na Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Ndama Bw Erenest Mabula wamesema kuwa mila na desturi za zamani ndizo tu ambazo kwa sasa zitasaidia kuwabadilisha watoto wa kike kwani maadili yao yameporomoka kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na miaka iliyopita.
Wameongeza kuwa mila na desturi za zamani zikitumika kikamilifu katika kuimiza maadili kwa vijana tatizo hilo litakwisha kwani hata walipokuwa wadogo malezi yalikuwa mazuri na kuwa hali ilivyo hivi sasa ni tofauti na zamani ambapo kulikuwa na adhabu kali zilizokuwa zikichukuliwa kwa wanaobanika kuwa na mimba.
Bw Gorge Rumanyika ambaye ni mratibu Elimu kata ya Ndama amebanisha kuwa njia zinaweza kusaidia kutokomeza tatizo hilo ni pamoja na jamii nzima kuwajibika katika kukemea vitendo viovu vya ngono kwa watoto wao.
Aidha wameongeza kwamba hivi sasa uongozi wa kata upo katika harakati za ujenzi wa mabweni unaotarajia kuchangia kwa kiasi kikubwa kumaliza kero hiyo kwani watoto watakuwa chini ya uangalizi mzuri kiliko hivyi sasa wanavyoishi kwenye vyumba vya kupangisha.
Katika kufuatilia maisha wanayoishi wanafunzi wilani Karagwe uchunguzi uliofanywa na timu ya waandishi wa Habari chini ya shirika la UTU Mwanamke umebaini kwamba,wanafunzi walio wengi wanaishi katika vyumba vya kupanga kitu kinachosababisha kuwepo kwa vishawishi vya ngono kwa baadhi ya watoto wa kike.
Wanafunzi hao walipo ulizwa ni kwa nini wanaishi kwenye vyumba hivyo wamesema kwamba maisha ya kupanga uraiani ni rahisi kwani kwa mwezi wanalipia chumba sh.5,000 kitu ambacho hata wakijengewa hosteli wazaza wao hawataweza kuwalipia gharama za kukaa huko kwani kipato chao ni kidogo.
Hata hivyo utaratibu huo unapigana na mkakakati wa mkuu wa wilaya ya Karagwe Kanal Fabian Masawe kuwa wanafunzi wote wanaoishi kwenye nyumba za kupanga wahame mara moja.
Baadhi ya wanafunzi hao waliohojiwa kuhusiana na mkakati huo Beatrice Valentine,Adolf Munio na Wabura Kahunzwa wa shule ya sekondari Ndama wamesema kwamba kauli hiyo ya Masawe ni kuwanyima nafasi ya kusoma kwani wanapotoka ni mbali na shule hivyo wakifukuzwa katika maeneo hayo wataacha shule.
Wameongeza kuwa wao wanapangisha ili kupunguza umbali uliopo ambao wamesema ni wa mwendo wa masaa mawili hivyo,wao hataondoka na badala yake wanamuomba Masawe haitishe kikao na wazazi wao ambao ndio wamewaruhusu kupangisha vyumba hivyo.
Wamefadanua kuwa tatizo hilo litakwisha endapo tu wataweza kupata mahitaji yao yote toka kwa wazazi wao.
Takwimu zilizotolewa na mkuu wa wilaya ya Karagwe Kanal Fabian Masawe kuhusiana na tatizo la mimba mashuleni ni kuwa kwa mwaka 2008 wanafunzi 102 wa shule za sekondari na msingi walibebeshwa mimba,mwaka 2009 waliobebeshwa mimba walikuwa 45 na mwaka huu hadi kufikia sasa ni wanafunzi 20.
MWISHO.