UNYANYAPAA UNATUUA MAPEMA WAVIU.
N Hassan Simba, Lindi.
Julai 12, 2010. KUWAPO kwa tabia ya unyanyapaa miongoni mwa jamii dhidi ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi mkoani Lindi, kumeelezwa kuwa kunachangia kuwakwaza kiuchumi na kuzorotesha afya zao na kusababisha wengi wao kupoteza maisha mapema richa ya kuanza kutumia dawa za kupunguza makali ya ugonjwa huo ARVs.
Hayo yamebinishwa juzi na watu wanaoishi na virus vya ukimwi mkoani hapa walipokuwa wakiongea kwa nyakati tofauti na waandishi wa habari waliokuwa katika utafiti dhidi ya unyanyapaa na unyanyasaji wa kijinsia, ulioratibiwa na chama cha wandishi wa habari za ukimwi nchini AJAAT kwa msaada toka kwa Watu wa Marekani (USAID), kupitia Futures Group International chini ya mradi wa Health Policy Initiative (HPI).
Amina Kondo, mmoja kati ya watu wanaoishi na virusi vya ukimwi ambaye amejiweka wazi kwa jamii, anasema kuwa unyanyapaa umesababisha baadhi yao kushindwa kuendelea na kufanya shughuli za kiuchumi na kubaki tegemezi huku wengine wakikatisha dozi kukwepa kunyoonyewa vidole na watu wanapokuwa katika vituo vya kuchukulia dawa.
“Mimi nimegundulika kuwa na virusi vya ukimwi tokea mwaka 2004 na kuanza kutumia dawa za ARVs…..lakni wenzangu wengi wameacha kutumia kukwepa kunyooshewa vidole na fya zao hivi sasa ni mbaya……na hata nilipoanza kufanya biashara ya kuuza mihogo watu wakataa kununua kwa vile eti nitawambukiza virusi”, alisema Amina.
Mama huyo mwenye watoto watatu na mbaye amepoteza mume kwa maradhi ya ukimwi. Na mkazi wa Lindi mjini, alisema kuwa kama asingekuwa na ujasiri wa kujitangaza na kuwa wazi kwa jamii ingemuiya vigumu kuendelea na shughuli zake na kutumia dawa hizo.
“Sasa wamezoea na wananunua mihogo kwangu…nadhani upo umuhimu wa watu tuliona virusi hivi kuwa wazi maana hii inaweza kutupunguzia msongo wa mawazo…..na hawa wanowanyooshea vidole wenzao wakapime wajue afya zao maana wengi wao hawajapima”, alisema Amina.
Naye Geoge Simba, mwanachama mwanzilishi wa kikundi cha uzalishji kipato cha watu wanaoishi na virusi vya ukimwi wilayani Kilwa, alisema kuwa licha ya kikundi chao kuwa na wanachama 26 lakini walioamua kuw wazi na kujitangaza kwa jamii ni wane tu huku wengine wkihofu kunyanyapaliwa.
Simba baba wa mtoto mmoja alisema kuwa alipojitangaza kuwa naishi na virusi jamii ya wakazi wa Kijiji cha Ngulukulu anapoishi na kufanya biashra zake walimtenga na kuacha kununua bidhaa zake kwa kuhofia kuambukizwa.
“Mimi na mke wangu tumekuwa tukiishi na virusi vya ukimwi kwa zaidi ya miaka tisa sasa…..lakini mwanzoni tuliyumba sana baada ya jamii inayotuzunguka kutunyanyapaa na kama nisingekuwa jasiri n kusimma imara katika biashara zangu za chips na kuku hali zetu zingezidi kuwa mbaya” lisema Simba.
Mganga mkuu wa mkoa wa Lindi, Dk. Mohamedi Alli, aliwaambia waandisi wa habari kuwa waganga katika hospitali na vituo vyote vya kutolea huduma mkoani umo wamepewa mafunzo yanayowawezesha kuwahudumia wagonjwa wote wkiwemo wale wanaoishi na virusi vya ukimwi ili kuondoa unyanyapaa.
“Hapa katika hospitali ya mkoa tumeweka kituo kimoja ambapo mtu anayeishi na viru vya ukimwi anpta huduma zote…..lakini pia vituo vyote vya kutolea huduma mkoani kwetu waganga wanawahudumia wote hakuna tena utaratubu wa kuwatengea….hii inasaidia kuondoa unyanyapaa …lakini hii ni kwa upande wa afya na ukimwi ni suala mtambuka na wemgine waitmize wajimu wao hili si suala la kihospitali tu” alisema Dk Mohamedi.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment