Na Ramadhan Libenanga , Morogoro .
Makala .
Familia nyingi nchini zimekuwa na tatizo la watoto wengi kushindwa kupata elimu ya msingi na hata huduma muhimu wakiwa kama watoto ndani ya familia .
Mwandishi wa makala hii fupi amebaini ni hili katika familia nyingi wilayani Mvomero kutokana wazazi wao kutofuata uzazi wa mpango katika familia zao na hivyo kupelekea kuzaa watoto zaidi ya 8.
Bi Hadija Suleiman mkazi wa Embeti (34) wilayani Mvomero mwenye watoto tisa anaelezea sababu kubwa za familia nyingi kuwa na hali duni kimaisha kutokana na kutokuwa na elimu kuhusu masuala ya uzazi wa mpango.
Ambapo anasema kuwa yapo mambo mengi sana yanayosababisha wakina mama wengi kushindwa kutumia njia ya uzazi wa mpango .
Alisema kuwa yapo matatizo ya itikadi za kidini kwa waume zao , ukilitimba ,na ubabe wa waume zao kutokana na ukosefu wa elimu dhidi ya uzazi wa mpango .
Hata hivyo mama huyo anadai kuwa kundi la wanaume wengi bado halina elimu ya kutosha kuhusu mpango mzima wa uzazi wa mpango na hivyo kuwa chanzo kikubwa katika kufanikisha zana nzima ya uzazi wa mpango .
“inapofikia mwanaume akagundua mwanamke umefunga kizazi kwa njia yeyote bila kumshirikisha , basi utapokea kipigo na hata kupoteza ndoa yako “ alisema mama huyo.
Aidha pia mama huyo anadai kuwa pia imani na uzushi uliopo mitaani kuhusu njia hizo za uzazi wa mpango , uwenda ukawa chanzo kikubwa cha wanawake na waume kukataa kujiunga na aina hizo za uzazi wa mpango .
Hata hivyo naye mganga mkuu msaidizi katika hospitali ya Mission ya Bwagala wilayani Mvomero , Bw Mashaka Shemkande .
Bw Shemkunde alikiri wakina mama na wakina baba katika wilaya hiyo bado hawana elimu ya kutosha kuhusu uzazi wa mpango.
Ambapo alisema kuwa kutokana na hali hiyo ndio sababu kubwa inayopelekea kuwepo na vifo vingi vinavyotokana uzazi wa mara kwa mara , ikiwa pamoja na watoto kuzaa kabla ya umri .
Alisema kuwa kwa kipindi cha mwezi januari mpaka mei tayari hospitali hiyo imepokea watoto 1226 waliozaa kabla ya umri wakiwa na miaka kati ya 15 mpaka 16 .
Hata hivyo alisema kuwa hospitali hiyo imejikuta ikipokea wagonjwa wengi kuliko uwezo hasa wenye kesi zinazotokana , ukosefu wa elimu kuhusu uzazi wa mpango .
Mwisho
No comments:
Post a Comment